• Breaking News

    Walemavu na Maendeleo Tanzania

    mmoja wa mwanafunzi kijana,aliyewezeshwa kupata msaada wa baiskeli ili kumuwezesha kufika shuleni kwa urahisi(PICHA KWA HISANI YA WEBSITE YA TEA)

    Ukikaa chini na kutafakari kwa kina,kwanini kuwekuwa na changamoto za kila siku zinazozungumzia vijana  na maisha yao ili kufanya kijana ajitambue yeye ni nani,utakubaliana nami kuwa zinahitajika sana katika jamii ya vijana.Makampuni mbalimbali ya watu binafsi na taasisi za dini,zikijihusisha na shughuli kama hizi pamoja na serikali ambayo nayo inajitahidi katika kuinuia vijana walemavu katika masuala mbalimbali.
    Serikali yetu kwa hivi sasa kupitia wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi chini ya waziri mwenye dhamana,Dr.Shukuru Kawambwa kupitia taasisi yake ya TEA(TANZANIA EDUCATION AUTHORITY) iliyopo millenium tower,jijini Dar es salaam,wanamkakati maalumu ambao una madhumuni ya kuinua vijana walemavu kupata elimu bora.Vijana walemavu ni wengi sana wanaotuzunguka katika jamii yetu.Wengine ni ndugu zetu ndani ya jamii zetu.
    Kitu pekee kinachoweza  kuwasaidia vijana walemavu ni kupata elimu ya


    kujitegemea na kufanya kazi zao binafsi,kwa kuwawezesha vijana walemavu kwa elimu ya kujitegemea ,tutapunguza tatizo kubwa la ombaomba na watu walio walemavu katika barabara zetu,na mitaani.Dunia hii ya utandawazi na kila kinategemea elimu.kamavijana walemavu wakielimishwa basi tutakuwa tumepunguza wimbi la umaskini kwa kiasi kikubwa maana ombaomba walemavu watapungua.

    Mbunge kijana,ambaye ni mlemavu mh,Regia Mtamanyenja akiwakilisha vyema bungeni na mfano wa kuigwa kwa vijana wengine walemavu ili waweze kufika mahali alipofika

    Pia jamii nzima inabidi itambua jukumu kama hili ni la watu wote,kwa kuwawezesha walemavu Tanzania nzima.Naamini ni lengo la kila mtanzania kuona umaskini unapungua kwa kiasi kikubwaili kuinua uchumi wetu hapa nchini.Walemavu wanaweza kama waliwezeshwa kupata elimu bora,kama mh.RegiaMtemanyenja mbunge wa Kilombero.ambaye ni kijana ,ameweza kauwakilisha jimbo lake hali ya kuwa ana ulemavu,hii ni sababu alipata elimu tosha.hivyo kama mtanzania mwenye uchungu wa kuona vijana walemavu wakitanzania wanaendelea ,basi nawe wekeza katika elimu ya walemavu ili kuwainua walemavu wa hapa nchini.
    Kama kijana wa kitanzania na sera yetu iwe kuwa kijana mlemavu anaweza akiwezeshwa,kwa kupewa changamoto mbalimbali na sio kuwaachawakiwa ombaomba bila ya msaada na tegemzi katika jamii.Jitoekwa kujenga shule,nunua mavazi,toa mchango wowte ule katika taasisi mbalimbali zinajihusisha na masuala ya kusaidia vijana walemavu ili waweze kupata elimu bora na ya kujitegemea popote pale wanapokuwa.Fanya hivyo mara zote ili kulisongesha kurudumu la maendeleo ya Taifa la Tanzania.VJANAWALEMAVU WAKIWEZESHWA WANAWEZA

    1 comment:

    1. Titanium Tent Table - Hot - Titsanium Art
      Titsanium Art. cost of titanium Titanium titanium damascus tent table with the option titanium mokume gane to start the game without any unnecessary labor. Titsanium, the titanium flat irons most popular form of paint and  Rating: is titanium a metal 4.2 · ‎8 reviews

      ReplyDelete