• Breaking News

    Elimu Jumuishi ni mkombozi kwa walemavu-SHIVYAWATA


    Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), kimeitaka serikali kufanya jitihada za kuwa na elimu jumuishi.

    Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), kimeitaka serikali kufanya jitihada za kuwa na elimu jumuishi badala ya hivi sasa ambapo hakuna usawa katika elimu kati ya walemavu na wasio walemavu kwa kuzingatiwa kuwa miundombinu ya watu wenye ulemavu iliyopo nchini haikidhi matakwa na vigezo vya utoaji wa elimu.
    Akitoa wito huo katibu mkuu wa SHIVYAWATA Felician Mkude amesema kuwa kutokana na changamoto zilizopo kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania serikali iliweka utaratibu wa kuwepo kwa shule maalum za walemavu lakini suala hilo sasa limegeuka kuwa mwanzo wa kutengwa kwa watu wenye ulemavu.
    Mh. Mkude amefafanua kuwa hali ya kuwawekea walemavu shule zao maalum sio mbaya ila ukweli wa sasa ni kwamba, walemavu wamekuwa wakitengwa katika nafasi mbalimbali za ajira na hata uongozi.
    SHIVYAWATA imetaka sasa katika shule zote kwa dhana ya elimu jumuishi iwekwe miundombinu ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kujumuika na wanafunzi wengine ili kuzoeana na kuweka usawa.

    No comments