• Breaking News

    HISTORIA YA WAKONTA KAPUNDA.


    MSICHANA Wakonda Kapunda mwenya umri wa miaka 25 anateseka baada ya viungo vyake kupooza kufuatia ajali ya gari iliyompata akiwa shule ya sekondari ,korogwe Tanga.


    Akisimulia kisa kizima kwa Uwazi na maisha yake kwa ufupi akiwa nyumbani kwao,Rukwa ,Wakonta anasema "Mimi naitwa Wakonta Kapunda ,Naishi mkooa wa Rukwa.

    "Nilipomaliza elimu ya msingi ,nilifanikiwa kujiunga na sekondari ya Wasichana Korogwe.Ilikuwa wakati najiandaa kufanya mtihani wa mwisho.

    "Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012,ndipo nilipopata tatizo hili.Ilikuwa siku ya mahafali{gradution}yangu ,mwezi wa pili mwaka huo tukiwa tunajiandaa,mmoja wa wanafunzi aliwasha gari na kuweka reverse kwa kasi hivyo kunigonga mimi pamoja na baadhi ya wanafunzi.



    Gari lililomgonga Wakonta kapunda siku ya mahafari.


    "Hapo  ndipo ulikuwa mwanzo wa safari yangu ambayo sijawahi hata kuifikiria kwani nilivunjiaka uti wa mgongo na kupooza kutoka mabegani mpaka miguuni.

    "Katika kutibiwa ,ilibidi nipelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji lakini bila mafanikio.

    "Kuanzia hapo nikawa mtu wa kukaa na kulala tu.Nilijaribu kuyafikiria maisha yangu ya baadae nikawa naona giza nene mbele.



    "Ilifika mahali nikakata tamaa ya maisha lakini Mungu alinisaidia ,alinitia nguvu na kunifanya nikubaliane na hali halisi.Najikubali nilivyo na ndio maana naweza kufanya mambo ambayo ,wengine wanashangaa sana .mfano ,namiliki simu ya kisasa[smartphone] lakini uwezo wa kuitumia sina,inabidi nitumie ulimi kuandikia kwa vile vidole havifanyi kazi inayotakiwa.

    Mwaka 2016 lilitokea shindano la kuandika filamu [script],Shindano ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya Filamu ya Maisha ya nchini Uganda. Wakonta aliweza kushinda  hatua ya kwanza ya shindano hilo ambapo aliandika filamu [script] kwa kutumia ulimi.

    Wakonta hakuweza kuibuka kidedea katika shindano hilo lakini alijitahidi kuendeleza kipaji chake cha uandishi wa filamu ,

    Anasema japo kuwa amepooza mwili wote lakini hajakata tamaa,anaamini ipo siku moja atapona ,Pia amesema kuwa ,madaktari walimuambia hawajui ni hospitali gani inaweza kumponesha hivyo kumkatia tamaa kwamba hakuna uwezo wa kuwa sawa tena.

    Wapo binadamu wenye viungo vilivyokamilika lakini wanashindwa kuvitumia kufanya kazi za kuingiza kipato.

    Hii ni tofauti kwa Wakonta kapunda ambae kwa kutumia kichwa chake pekee,kikiwa ni kiungo kimoja kinachofanya kazi katika mwili wake ,amekuwa na uwezo wa kuandika filamu [script] na kuahidi kuendelea kuitumikia jamii yake .

    Wakonta ni msichana mwenye udhubutu ,licha ya matatizo aliyonayo aliona kuna kitu anweza uifanyia jamii, wakonta alishiriki katika mafunzo ya uandishi wa muswada ya Maisha Lab ,Visiwani Zanzibar ,Kubwa zaidi  ikiwa ni mbinu alizozitumia kung'amua jinsi ya kutumia simu kwa njia ya ulimi,Wakonta alizungumzia mafanikio yake kwa kushirirki mafunzo ya uandishi wa muswada. 

    Wakonta alizugumza maneno haya"

                         "Mafanikio yangu ni makubwa na nina furahi sana kwa hatua ambazo nimezifikia japo kuwa bado sijafanikiwa kuandika filamu,lakini nimejifunza mengi,nimefanikiwa kuwa katika nafasi nzuri ,nimejua namna ya kuandikia muswada,wahusika katika kazi yangu na mengin mengi ambayo awali sikuyafahamu.


    Video: JINSI ALIVYOJIFUNZA KUANDIKA KWA ULIMI. 





    "Nilijifunza nikiwa nyumbani wakati huo mdogo wangu aliniachia simu kwa bahati mbaya au nzuri ile simu ikaita,simu ilikuwa karibu na mwili sasa wakati nahangaika kuipokea nikaigusa gusa ile simu ikakubali ikajipokea,nikagundua kitu kumbe simu ukiigusa hata kwa mwili inakubali ,siyo kidole pekee.

    "Mdogo wangu alipoamka nikamwambia tufanye namna hii simu inifikie,akaishirikisha familia wakakubali wakaniwekea mito na vinginevyo nikaweza kuitumia ,nadonoa taratibu,awali kichwa kiliniuma,kizunguzungu,ulimi uliniuma ila nilifanya kila siku nikazoea.kwa sasa nina spidi nzuri ninafanya kazi kubwa kupitia ulimi wangu ninaandika siku nzima .

    JINSI ALIVYOWEZA KUANDIKA MUSWADA WA FILAMU NA MBINU ALIYOTUMIA KUPATA  NAFASI ALIYO NAYO.


    "Nimejifunza nyumbani ,nilikuwa sijui muswada unaandikwaje nikajifunza kupitia nyumbani.
    Nilianza kuingia katika mitandao kuangalia waandishi wa Nollywood,Hollywood wanafanyaje ,nikadonoadonoa kila sehemu mpaka badae nikapata wazo na hilo wazo likanifanya niandike muswada ambao ndio nilitumia kwenye mashindano,nikachaguliwa kushiriki mafunzo. 


    SABABU ZILIZOMPELEKEA AINGIE KATIKA UANDISHI WA MUSWADA WA FILAMU.

    "Filamu zinauwezo wa kuendelea kugusa maisha yetu ya wakati ya jana ya leo yaliyopita na yajayo,kipidi naumwa nilikuwa naangalia filamu muda wote,kipindi hicho nilijua kwamba kupitia filamu unaweza kuhamasisha kubadilisha maisha yako na ukajua huzuni za watu.

    "Nikatamani niwe mmoja wa watua ambao wanawapa wengine farajana wale waliopo katika wakati mgumu wanapata faraja,unamha,asisha mtu unampa mwangaza mpya unamwonyesha maisha mazuri zaidi maana unaweza kusema una maisha magumu kumbe mwenzako ana wakati mgumu zaidi.

    CHANGAMOTO ALIZOKUTANA NAZO.
    "Changamoto zipo nyingi ila kwa kazi yangu kwa sasa hivi nikitaka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine lazima awepo mtu,lakini pia  kuandika kwa kuwa natakiwa kuwa nimekaa,hivyo nikiwa kitandani nashindwa kufanya chochote ,pia kifaa cha kuandikia nahithaji kupata simu nzuri zaidi itayoniwezesha kufanaya kazi zangu kwa urahisi.

    MAPOKEZI YAKE KWA WADAU WA FILAMU.
    "Nimejulikana kwa kipindi kifupi sana,nimekutana na watu wa bodi ya filamu wakanipokea na nikazungumza nao,wameniambia Tanzania kuna uhaba wa waandishi wa miswada,hivyo wamenipkea kwa mikona miwili,wakanichangia kiasi cha Tsh milioni  tano. Pia Shirirkisho la Filamu Tanzania[Taff] wameniahidi kwamba nikitoka kwenye mafunzo watanipa kazi za kufanya,wataniingiza rasimi kwenye taasisi yao.

    KIU YA WAKONTA KAPUNDA SIKU AKIKUTANA NA RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR.JOHN POMBE MAGUFULI 

    "Nikikutana na Raisi John Pombe Magufuli nitamwambia filamu zina nguvu ,Tanzania yetu itasonga mbele kupitia sanaa,Sisi waandishi,Wigizaji na ,Watayarishaji filamu tuna uwezo mkubwa.


    Wakonta hakukata tamaa na ndoto yake mpaka siku ambayo alijitokeza  mwanadada  ambae aliguswa kufanya kitu kumsaidia wakonta, Mwanadada Olivia Soko kutoka Afrika ya kusini ambae ni Mkurugenzi wa Whirlmarket Technologies company, Olivia alijitolea kutoa msaada wa programu ya kompyuta iitwayo Nuance Dragon Naturally Speaking ambayo ufanyaji kazi wake utakuwa ni pale mtumiaji anapokuwa anazungumza anachotaka kuandika kupitia kipaza sauti chake halafu programu hii inaandika yenyewe katika kompyuta ya mtumiaji.Ilikuwa ni furaha kwa Wakonta pamoja na familia yake.


     Wakonta  akitumia programu ya kompyuta {Nuance Dragon Naturally Speaking}

    1 comment:

    1. Tuna mengi saaana ya kujifunza. Huu ni sehemu ya muujiza Kati ya miujiza mingi ambayo binadamu tunaiwaza, kudhani na kuifikiria vichwani mwetu. Tatizo tuliowengi tunavyoifikiria miujiza sivyo ambavyo inatakiwa kufikiriwa au kudhaniwa. One day lazima nije kuonana na Wakonta uso kwa uso nitafurahi sana!

      ReplyDelete