• Breaking News

    Kutana Na Mwanaidi Mayowela: Mwanamke Mlemavu Mwenye Ndoto Za Kuwa mjasiliamali Mkubwa Baadae



    Mwanaidi mayowela Ni mwanamke  aliyekua anaomba omba maeneo ya posta kulingana na changamoto ya viungo vya mwili wake (ULEMVU). Baada ya kumtembelea  na kuongea na kwa kina ni kwa jinsi gani anaweza kujikwamua kimaisha kwa kutumia mikono yake, mwanamke huyu aliweza kuitikia wito huo na kujiunga na kikundi cha wamama wenzie waliokua wanajishuhulisha na kazi za mikono. 



    Mwanaidi mwayowela alionyesha nia ya kutaka kufanya biashara yoyote ambayo ingeweza kumsaidia, aliweza kuanza kutengeneza culture pamoja na mikoba ambaoyo alkua anauzia maeneo yale aliyokua anaomba omba. 
    Tuliendelea kumtembelea kuona maendeleo yake tukaona anaweza na ikapelekea akajiona na yeye anaweza kufikia malengo yake na akaacha dhana ya kuomba .

                                       

    Mwanaidi mayowela aliendelea kufanya biashara zake kwa umakini zaidi bila kujali changamoto alizo kua nazo na ikapelekea kuingia kwenye shindano lililo anzishwa na television  ya CLOUDS, lijulikanalo kama malikia wa nguvu.
    Mwanaidi alifanikiwa kuibuka  mshindi katika shindano hilo na ikamsababisha yeye kua na maisha mazuri na familia yake na akakumbuka kusaidia wengine. 

                                 

    Kutokana na changamoto alizokua nazo mwanaidi mayowela aliweza kukubali kushauriwa na kukubali kufanya kazi kwa kutumia mikono yake bila kujali changamoto ya miguu aliyo kua nayo. 




    Hi inaonesha kua na changamoto za mwili si sababu zinazo pelekea kuomba omba lakini unaweza kutumia uwezo ulionao kuweza kujikwamua kiuchumi. 

    "TANZANIA BILA WATU WENYE ULEMAVU INAWEZEKANA" 

    No comments